IQNA

Wairaki wafanya maandamano kuunga mkono harakati za mapinduzi ya Bahrain

13:54 - March 10, 2012
Habari ID: 2288849
Wananchi wa Iraq jana Ijumaa walifanya maandamano katika miji tofauti ya nchi hiyo kwa lengo la kuunga mkono matakwa ya wananchi wa Bahrain wanaofanya maandamano ya amani kwa ajili ya kufikia haki zao za kimsingi.
Maandamano hayo yamefanyika sambamba na yale ya Wabahrain wenyewe yaliyofanyika chini ya anwani ya kuitikia wito wa taifa la nchi hiyo. Wairaki wametaka kuondoka mara moja kwa askari vamizi wa Saudi Arabia nchini Bahrain. Mandamano hayo ambayo yalishuhudia mahudhurio makubwa katika miji muhimu ya Iraq na hasa ya Basra, Kut ma Nasiriya yalifanyika kujibu wito uliotolewa na Sayyid Muqdada Sadr. Kiongozi huyo wa kidini amepinga kila aina ya uingiliaji wa kigeni na hasa wa Marekani na nchi za Kiarabu nchini Bahrain kwa ajili ya kukandamiza harakati za Kiislamu katika nchi hiyo. Wakiongozwa na Ayatullah Isa Qassim, Kiongozi wa Mashia wa Bahrain, malaki ya Wabahrain walijitokeza na kushiriki kwa wingi katika maandamano hayo ili kujibu madai ya watawala dhalimu wa nchi hiyo kwamba ni idadi ndogo tu ya Wabahrain ndiyo inayoshiriki katika maandamano ya kupinga utawala huo. 968532
captcha