IQNA

Ombi la kufanyika maandamano ya kimataifa ya Quds

13:54 - March 10, 2012
Habari ID: 2288850
Shakhsia kadhaa wa kisiasa na kidini wametoa wito kwa walimwengu kushiriki kwenye maandamano makubwa ya kimataifa kwa lengo la kutetea Quds Tukufu.
Likitangaza wito huo, Baraza la Ushauri la Maandamano ya Kimataifa la Quds siku ya Alkhamisi lilitoa taarifa likiwataka watu wote duniani kushiriki katika maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika tarehe 30 mweizi huu wa Machi kwa kuzingatia njama za utawala haramu wa Israel za kuyahudisha Quds na kutekeleza mipango ya ubaguzi wa rangi katika mji huo mtakatifu. Taarifa hiyo ambayo imetiwa saini na shakhasia mashuhuri wa kimataifa wakiwemo Desmond Tutu, mshindi wa tuzo ya amani a Nobel, Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia, Ahmad Ubeidat, Waziri Mkuu wa zamani wa Jordan, Leith Shbeilat, mwanaharakati wa kisiasa na mbunge wa zamani wa nchi hiyo, George Galloway mbunge wa zamani wa Uingtereza na Marzouq Ali Spika wa bunge la Indonesia. Shakhsia hao wa kimataifa wametangaza ushirikiano wao kwa ajili ya kufanikisha maandamano hayo na wametaka suhula zote za kimataifa zitumike kwa lengo hilo. Taarifa hiyo inasema kuwa utawala wa Kizayuni umekuwa ukikiuka wazi misingi ya sheria za kimataifa kuhusiana na suala la Quds na kwamba sera zake za kuimarisha ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina katika mji huo ni suala linalokiuka wazi sheria za kimataifa za kuwataka wanadamu wote waishi pamoja kwa amani bila kuzingatia tofauti zao za rangi, dini wala utamaduni. Imeendelea kusema kuwa sera za utawala huo haramu zinalenga kuvuruga kabisa muundo wa kijamii na utambulisho halisi wa Kiarabu na Kiislamu katika mji huo. 968314
captcha