Jimbo hilo ni moja ya majimbo manne ambayo yamepitisha mswaada wa kufanya mafunzo hayo kuwa ya lazima. Viongozi wa majimbo hayo wana matumaini kwamba jambo hilo litasaidia kueneza mafundisho ya dini ya Kiislamu miongoni mwa wakazi wake. Kabla ya hapo ni juzuu chache tu za Qur'ani ndizo zimekuwa zikifundishwa katika shule hizo lakini kutokea sasa kitabu hicho kizima pamoja na tafsiri ya aya zake itakuwa ikifundishwa katika shule hizo. 968297