IQNA

Wanakaligrafia wa Iran na Uturuki kuandika nakala ndefu zaidi ya Qur'ani duniani

22:26 - March 10, 2012
Habari ID: 2289053
Wanakaligrafia wawili wa Iran na Uturuki wanashirikiana katika kuandika nakala ya Qur'ani Tukufu ambayo itakuwa ndefe zaidi duniani.
Shirika la habari la NUN la Iraq limeripoti kuw,a Halmashauri ya mji mtakatifu wa Najaf imeanza kazi hiyo ya kuandikwa nakala ndefu zaidi ya Qur'ani duniani kwa kushirikiana na Kamati ya Utungaji, Ubunifu na Uchapishaji ya mpango wa "Najaf, Mji Mkuu wa Ulimwengu wa Kiislamu Mwaka 2012" kwa ajili ya kuirikodi katika tabu la rekodi za dunia la Guinness.
Afisa anayesimamia Kamati ya Utunzi na Uchapishaji ya mpango wa Najaf, Mji Mkuu wa Ulimwengu wa Kiislamu" Hussein Ali Marzah amesema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani Tukufu itakuwa na urefu wa mita 5500 na upana wa mita moja.
Amesema kuwa dinari milioni 100 za Iraq zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo na uandishi wake utakamilika katika kipindi cha miezi saba. Ameongeza kuwa wanakaligrafia wawili kutoka Iran na Uturuki wanashirikiana katika kutekeleza kazi hiyo. 968939
captcha