IQNA

Nakala ya Qur'ani iliyoandikwa kwa hati za mkono katika maonyesho ya Riyadh

22:27 - March 10, 2012
Habari ID: 2289054
Nakala ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa hati za mkono mwaka 1112 Miladia inaonyeshwa katika chumba cha Austria katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu mjini Riyadh, Saudi Arabia kwa ajili ya kuuzwa.
Kituo cha habari cha shorouknews kimeripoti kuw,a nakala hiyo ya Qur'ani inaonyeshwa katika chumba chaAustria ambacho kinauza vitabu nadra kupatika vya lugha za Kiarabu, Kifarsi na Kituruki.
Nakala za baadhi ya vitabu vinavyouzwa katika chumba hicho ziliandikwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita. Nakana hiyo ya Qur'ani inauzwa kwa riali laki tatu za Saudia.
Nakala hiyo ya Qur'ani iliyonakshiwa kwa maji ya dhahabu iliandikwa kwa hati za mkono mwaka 1112 Miladia na inasemekana kuwa iliandikwa nchini Iran au Iraq.
Mmiliki wa chumba kinachouza vitabu hivyo vya kale katika maonyesho ya vitabu ya Riyadh anasema kuwa nakala hiyo ya Qur'ani ni ya aina yake. Michael anasema nakala mbili za aina hiyo zinaonyeshwa katika maonyesho hayo, moja ikiuzwa kwa riyali elfu 27 na nyingine inauzwa riali laki tatu.
Maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya Riyadh iliyoanza tarehe 6 Machi itaendelea kwa kipindi cha siku 10. 968634

captcha