Sherehe maalumu za kuadhimisha siku hiyo zilifanyika chini ya usimamizi wa chama cha Ahlul Hadith cha Lahore kwa kufanya maandamano ya kupinga kitendo hicho kiovu cha askari wa Marekani huko Afghanistan katika miji mbalimbali ya Pakistan.
Mjini Peshawar, Jumuiya ya Waislamu wa Pakistan (APML) iliitisha maandamano makubwa kwa mnasaba wa kuadhimisha siku hiyo na kupinga hatua ya askari wa Marekani ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu.
Kundi la Jaamat Daawat la Pakistan pia limeadhimisha siku hiyo kwa kufanya maandamano na kutoa wito wa kufikishwa mahakamani askari waliotenda uhalifu huo.
Mkuu wa kundi hilo Muhammad Hussein amelaani kitendo cha askari wa NATO cha kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu na ameikosoa serikali ya Pakistan kwa kunyamazia kimya kitendo hicho kiovu.
Sherehe za kuadhimisha siku ya Adhama ya Qur'ani zimefanyika katika miji mbalimbali ya Paksitan ambako maimamu wa Swala za Ijumaa pia wamelaani vikali kitendo cha kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu katika kambi ya askari wa Marekani huko Afghanistan. 968985