IQNA

Rais Ahmadinejad:

Iran na Iraq kuimarisha uhusiano zaidi

9:48 - March 11, 2012
Habari ID: 2289160
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran na Iraq zina hamu ya kuimarisha uhusiano wao licha ya njama za maadui za kuzuia ustawi wa nchi hizi mbili.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo Jana mjini Tehran alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Iraq Khudayr al-Khuzai. Rais Ahmadinejad amesema hakuna kizingiti katika uimarishwaji uhusiano wa pande zote wa Tehran na Baghdad katika nyanja za utamaduni, sayansi, teknolojia, nishati, maendeleo, biashara na uwekezaji.
Kwa upande wake Al-Khuzai ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misaada inayotoa kwa taifa la Iraq.
Akiwa Tehran, Makamu wa Rais wa Iraq pia amekutana na maafisa wa ngazi za juu wa Iran akiwemo Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu.
Uhusiano wa karibu wa Iran na Iraq ni kwa maslahi ya nchi hizi mbili kubwa za Kiislamu na maadui wakiongozwa na Marekani wamekuwa wakijaribu kuzuia umoja na ushirikiano wa nchi hizi mbili.
969039
captcha