Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, makaburi hayo ni mradi wa pamoja wa jamii za Waislamu Mashia na Masuni katika mji huo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Shirika la Makaburi ya Waislamu Canada amesema 'mradi huu wa makaburi ni hatua kubwa ya ushirikiano baina ya Waislamu wa madhehebu yote na jambo hili litaimarisha umoja wa Waislamu'.
Mmoja wa waanzishi wa mradi huo, Abdulhaq Ingar amesema mradi huo unajumuisha ardhi yenye ukubwa wa hekari 14 na imekadiriwa Waislamu wa Toronto watatumia makaburi hayo kwa muda wa karibu miaka 25.
Amesema sasa Waislamu wataweza kuzikwa kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu na kwamba makaburi yote yataelekea Makka.
968759