Baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limelaani vikali mashambulizi hayo na kuitaka jamii ya kimataifa kuilazimisha Israel ili isimamishe mashambulizi hayo.
Misri pia imelaani mashambulizi hayo ya kinyama ya jeshi la Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza na kutaka yasimamishwe mara moja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Muhammad Kamil Amru amesema Cairo ina wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo na inafanya jitihada kubwa za kusimamisha uchokozi huo.
Chama cha Amal Islami ambacho ni tawi la kisiasa la Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Jordan pia kimelaani mauaji ya kutisha yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Gaza na kimezitaka tawala rasmi za Kiarabu ziwasaidia wananchi wa Palestina.
Taarifa ya Amal Islami imesema adui Mzayuni hawathamini watu wasiokuwa Mayahudi kutokana na ada yake ya kibaguzi na kila siku anazidi kufanya jinai na mauaji mapya.
Mkuu wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu mashambulizi ya sasa ya Israel dhidi ya raia wa Ukanda wa Gaza na kusema Umoja wa Ulaya una wasiwasi kuhusu machafuko ya sasa huko kusini mwa Palestina. Ashton amesisitiza juu ya kokumeshwa mashambulizi hayo.
Ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zimekuwa zikishambulia maeneo ya raia wa Gaza tangu Ijumaa iliyopita. 969340