IQNA

Aya za Qur'ani kupamba metro za Marekani

14:52 - March 11, 2012
Habari ID: 2289737
Jumuiya ya Kiislamu ya Boston imechukua hatua ya kupachika mabango yenye maandishi ya aya za Qur'ani Tukufu katika vituo vya treni za chini ya ardhi maarufu kwa jina la metro kwa shabaha ya kupambana na propaganda chafu zinazofanywa dhidi ya Uislamu na kudhihirisha sura halisi ya dini hiyo ya Mwenyezi Mungu.
Tovuti ya Mooslym imeripoti kuwa, baada ya kufanikiwa mpango wa kulingania Uislamu uliopewa jina la "Usiuogope Uislamu, Utambue", Jumuiya yaKiislamu ya mji wa Boston nchini Marekani imeanzisha mpango mpya uliopewa jina la "Uislamu 101".
Mpango huo umeanza kutekelezwa katika metro za Boston kwa kuweka mabango na matangazo yanayobeba ujumbe wa aya za Qur'ani Tukufu na dini ya Kiislamu.
Moja ya mabango hayo lina tarjumi ya aya ya 34 ya Sura ya Fussilat inayosema: "Mema na maovu hayalingani. Ondoa uovu kwa kutenda lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki wa karibu wa kukuonea uchungu." Maandishi ya aya hii ya Qur'ani yamewavutia Wamarekani wengi wanaotaka kujua vyema dini tukufu ya Uislamu.
Jumuiya ya Kiislamu ya Boston ina nia ya kutekeleza mpango huo wa "Uislamu 101" katika maeneo ya metro katika miji mingine ya Marekani. 969824
captcha