IQNA

Kusikiliza qiraa ya Qur'ani huwasaidia wagonjwa

14:15 - March 12, 2012
Habari ID: 2290337
Qiraa ya Qur'ani Tukufu huimarisha mfumo wa kinga mwilini na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika kuponya mgonjwa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wanafunzi wawili wa chuo kikuu nchini Iran, qiraa ya Qur'ani Tukufu ina nafasi kubwa katika kuimarisha hali ya kiafya ya wagonjwa wa maradhi mbalimbali kama vile saratani.
'Taathira ya Qur'ani Katika Wagonjwa' ni anwani ya utafiti uliofanywa na Mustafa Tarkhasi anayesoma afya ya kimazingira akishirikiana na Majid Alizadeh ambaye anasomea Uuguzi.
Mustafa Tarkhasi amemwabia mwandishi wa IQNA kuwa, 'hisia ya matumaini na kujiamini hujitokeza katika wagonjwa ambao wanasikiliza Qur'ani Tukufu. Natija ya hali hili ni kuwa mfumo wa kinga huimarika na hivyo kipindi cha maumivu hupungua'.
Wanafunzi hao wamesema Qur'ani Tukufu ni muujiza na kuongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni watafiti wengi katika sekta ya tiba wanafanya uchunguzi zaidi kuhusu uwezo wa kitiba za Qur'ani Tukufu.
Wanafunzi hao wawili wanasema Qur'ani Tukufu ni kitabu cha muongozo ambacho kikifuatwa basi kinaweza kuponya na kuimarisha afya.
969596
captcha