IQNA

Mawahabi wateketeza msikiti na kumuua Imamu Ubelgiji

16:37 - March 13, 2012
Habari ID: 2290920
Imamu wa Msikiti wa Imam Redha AS Ubelgiji ameuliwa kikatili na watu wanaosadikiwa kuwa na itikadi za Kiwahabi katika mji mkuu wa nchi hiyo Brussels.
Kwa mujibu wa tovuti ya tf1, Bi. Isabelle Praile Naibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Ubelgiji amesema, 'siku ya Jumatatu tarehe 12 Machi Msikiti wa Imam Redha AS uliteketezwa kwa moto na watu wenye misimamo mikali ya Kiwahabi'.
Bi Praile ambaye pia ni kati ya viongozi wa Kishia nchini Ubelgiji amesema: 'Msikiti wa Imam Redha AS ni moja kati ya vituo muhimu zaidi vya ibada vya Waislamu wa madhehebu ya Shia na kwa miaka kadhaa sasa kutokana na vitisho vya Mawahabi, msikiti huu umekuwa ukilindwa na polisi'.
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo la kusikitisha amesema: 'Karibu saa moja usiku Jumatatu, watu waliushambulia Msikiti wa Imam Redha AS na kutupa bomu aina ya 'molotov cocktail' (bomu ya petrol) ndani ya msikiti na ukaanza kuteketea kisha wakafunga milango yote na baada ya hapo Imamu wa Sala ya jamaa pamoja na muumini mwingine walikufa shahidi kutokana na moshi'. Imamu aliyeuawa shahidi ametajwa na waumini wa msikiti huo kuwa ni Sheikh Abu Zainab aliyekuwa na umri wa miaka 39 na ambayo alikuwa anapendwa na watu wote kutokana na maadili yake mema.
Bi. Isabelle ameongeza kuwa: 'Moto huo umeteketeza maeneo yote ya msikiti huo na sasa hauwezi kutumika'.
Polisi nchini Ubelgiji wametangaza kuwa tayari wamewakamata watu wanaoshukiwa kuhusika na kitendo hicho cha jinai.
Meya wa eneo la Anderlecht mjini Brussels, Gaetan Van Goidsenhoven ametoa wito wa utulivu.
971046
captcha