IQNA

Waislamu Uingereza wanataka mfumo wa sheria za Kiislamu

16:56 - March 13, 2012
Habari ID: 2290938
Waislamu wanaotaka mfumo wa sheria za Kiislamu utekelezwe Uingereza wamezidi kuongezeka na wengi sasa wanaenda katika mahakama zilizopo za Kiislamu.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maelfu ya Waislamu Uingereza sasa wanafadhilisha kesi zao zisikilizwe katika mahakama rasmi zinazotoa hukumu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Citivas, mwaka 2009 kulikuwa na karibu mahakama 85 za Kiislamu mjini London.
Sheikh Haytham Haddad mmoja kati ya majaji katika Mahakama za Kiislamu Uingereza amesema: 'Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, idadi ya watu wanaotaka matatizo yao ya kisheria yatatuliwe katika mahakama hizi za Kiislamu imeongezeka mara tatu".
Sheikh Haytham ameongeza kuwa jambo hili linaonyesha kuwa leo zaidi ya huko nyuma Waislamu wanataka mfumo wa sheria za Kiislamu na wanaifahamu vyema dini yao.
Mahakama za Kiislamu nchini Uingereza zilianza kufanya kazi mwaka 1982 chini ya usimamizi wa mabaraza ya kieneo na kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo.
Nchi kadhaa za jumuiya ya madola zimeshaanzisha mahakama za Kiislamu ambazo Afrika Mashariki zinajulikana kama 'Mahakama za Kadhi'.
970485
captcha