IQNA

Bunge la Misri lataka balozi wa Israel atimuliwe nchini humo

16:42 - March 13, 2012
Habari ID: 2290949
Bunge la Misri siku ya Jumatatu 12 Machi usiku lilitoa taarifa kufuatia hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kutaka balozi wa utawala huo haramu atimuliwe Cairo mara moja.
Kwa mujibu wa tovuti ya Al Misr al Youm, Bunge la Watu wa Misri katika kikao kilichoongozwa na Spika Mohammad Saeed Al Katatni pia lilibuni kamati maalumu ya kufuatilia takwa hilo ili kuishurutisha serikali ya kijeshi nchini humo kulitekeleza
Wabunge wa Misri amesema wananchi wanamapinduzi wa Misri hawataki kua muitifaki wa utawala wa Kizayuni ambao ni adui mkubwa wa Misri na Umma wa Kiislamu. Aidha katika taarifa yao Wabunge wa Misri wametangaza kuunga mkono taifa linalodhulimiwa la Palestina na wametaka nchi za Kiarabu zikate uhusiano na utawala haramu wa Israel. Pia wametaka nchi za Kiarabu kuongoza mkakati wa kususiwa bidhaa za Israel duniani.
Jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina zimeongezeka sana katika siku za hivi karibuni. Mauaji ya kinyama ya utawala wa Kizayuni yanaendelea dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina huku jamii ya kimataifa ikiendelea kunyamazia kimya jinai hizo. Awamu mpya ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yalianza siku ya Ijumaa na hadi Wapalestina zaidi ya 20 wameshauawa shahidi wakiwemo watoto na wanawake.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema kuwa, mashambulizi hayo mapya ya Israel dhidi ya Wapalestina yana baraka kamili kutoka kwa Marekani hasa kwa vile mashambulizi hayo mapya yameanza siku chache tu baada Rais Barack Obama kuonana na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, mjini Washington, Marekani.
Wazayuni wanataka kuwaonesha walimwengu kuwa bado wana nguvu, hususan kutokana na kushindwa mara kwa mara na muqawama wa Palestina katika miezi ya hivi karibuni. Jambo jengine lililowafanya Wazayuni wazidishe jinai zao huko Gaza ni kujaribu kufunika mgogoro mkubwa unaoumeng'enyua na kuutafuna ndani kwa ndani kama mchwa, utawala huo dhalimu.
Hata hivyo Wapalestina wameapa kuendelea na muqawama na mapambano yao dhidi ya Wazayuni na ni jambo lililo wazi kwamba kuendelea jinai za Israel kutazidi tu kuwaamsha walimwengu na kuwaonesha sura halisi ya ukatili wa kufurutu ada ya utawala ghasibu wa Israeli.
971128
captcha