Kwa mujibu wa tovuti ya Ahram, Ahmad an-Nafis, kiongozi wa Mashia wa Misri ambaye pia ni mkuu wa chama kipya cha at-Tahrir amesema katika kipindi kimoja cha televisheni ya Sauti ya Taifa kwamba jambo hilo ni muhimu sana na hasa kwa kutilia maanani kwamba taasisi muhimu ya Kiislamu ya al-Azhar inatambua rasmi madhehebu ya Shia. Ameongeza kwamba Mashia hawafuatilii suala la kuwa na viti katika Baraza la Kutunga Katiba bali wanataka haki zao ziheshimiwe na kutobaguliwa nchini, kama ambavyo haki za Masuni zinalindwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Amesema Mashia ni Waislamu kama walivyo Waislamu wa madhehebu nyinginezo za Kiislamu ambao wanafuata kitabu kimoja cha Qur'ani kama walivyo Waislamu wengine. Amesema Mashia wa Misri wanataka kuheshimiwa haki zao za kiraia na kutobaguliwa katika nchi yao kama ilivyokuwa ikifanyika katika katiba iliyopita.
Mwanaharakati huyo wa Kishia amesema chama kipya cha at-Tahrir si chama cha kimadhehebu wala kikabila bali ni cha kisiasa kinachozingatia matakwa na maslahi ya makundi yote ya nchi hiyo. 971348