IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur'ani ya al Kauthar kuenziwa

17:50 - March 13, 2012
Habari ID: 2291273
Washindi wa mashindano yaliyoandaliwa na Kanali ya Televisheni ya Kimataifa ya al Kauthar wataenziwa Alkhamisi ijayo katika sherehe itakayofanyika kwenye Haram ya Hadhrat Maasuma (as) katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Kwa mujibu wa ofisi ya Televisheni ya Satalaiti ya al Kauthar, washindi wa mashindano ya duru ya nne ya Qur'ani Tukufu yaliyopewa jina la "Hakika Wamchao Mungu Wamefuzu" yaliyotayarishwa na kanali hiyo wataenziwa katika sherehe itakayofanyika mjini Qum.
Sherehe hiyo itakayowashirikisha washindi bora tano kutoka Misri, Iraq, Pakistan na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itahudhuriwa na maulamaa, shakhsia wanaojishughulisha na masuala ya Qur'ani na wadau wa masuala ya utamaduni.
Ofisi ya Televisheni ya al Kauthar imeyaalika mashirika ya habari, waandishi na wapenzi wa Qur'ani kushiriki katika sherehe hiyo.
Imesema ina matumaini kwamba sherehe hiyo itasaidia jitihada za kutukuza na kustawisha utamaduni wa Qur'ani hususan katika kipindi hiki ambapo maadui wa Uislamu wanakivunjia heshima kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu. 971449
captcha