Kwa mujibu wa tovuti ya Champress muungano huo pia umetaka kuimarishwa propaganda za vyombo vya habari kwa lengo la kuwalazimisha wavamizi wa Saudia kuondoka katika nchi yao.
Siku ya Jumanne tarehe 13 Machi sambamba na kutimia mwaka mmoja tokea askari vamizi wa Saudi Arabia waingie nchini Bahrain kwa lengo la kukandamiza harakati za mapinduzi ya nchi hiyo, Wabahraini wamefanya maandamano makubwa katika pembe zote za nchi hiyo wakitaka wavamizi hao waondoke mara moja katika ardhi yao.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wabunge wa Kuwait wamewatuhumu askari vamizi wa Saudi Arabia kuwa kukiuka wazi wazi haki za watu wa Bahrain, watu ambao wamekuwa wakifanya maandamano ya amani kutetea haki zao.
Wabunge hao wa Kuwait wamesema wanataka kuonana na wakuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ili kujadiliana nao kuhusu kadhia ya Bahrain. 971489