Kwa mujibu wa tovuti ya al-Alam, wito huo umetolewa katika hali ambayo Jumuiya ya Haki za Kiraia na Kisiasa ya Saudia imetoa taarifa ikisema kuwa makumi ya wanaharakati wa kisiasa na haki za binadamu wa nchi hiyo tayari wametangaza kususia chakula katika siku za al-Khamisi na Ijumaa ili kufungamana na wafungwa wa kisiasa wa nchi hiyo.
Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la nchi hiyo pia wamepanga kugoma kulalamikia ubadhirifu wa fedha na uongozi mbaya wa shirika hilo.
Akibainisha suala hilo, Dakta Anwar Ashqi, mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratijia cha Mashariki ya Kati amesema kwamba licha ya kuwa wananchi wa Saudia wamekuwa wakitumia njia za amani na za kiustaarabu kupigania haki zao kutoka kwa watawala wa Saudi Arabia lakini watawala hao wamekuwa wakitumia mkono wa chuma dhidi yao.
Dakta Ishqi ameongeza kuwa askari usalama wa nchi hiyo walitumia mabavu na kumuua binti mmoja na kuwajeruhi wanachuo wengine kadhaa katika Chuo Kikuu cha Mfalme Khalid katika mji wa Abha kusini magharibi mwa nchi hiyo, jambo ambalo limewakasirisha sana wanachuo wa chuo hicho. 971777