Gazeti la Oman News limeripoti kuwa, watu wanaotaka kushiriki mashindano hayo walikuwa na fursa ya kujiandikisha hadi leo Jumatano.
Mashindano hayo yatafanyika katika nyanja tano za hifdhi na tajwidi ya Qur'ani nzima, hifdhi na tajwidi ya juzuu 24, hifdhi na tajwidi ya juzuu 18, hifdhi na tajwidi ya juzuu 12, na hifdhi na tajwidi ya juzuu 12.
Washindi wa duru hii ya mashindano ya Qur'ani watachuana tena katika duru ya mwisho itakayofanyika hapo baadaye.
Duru ya 21 ya mashindano ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu ya Oman ilifanyika mwaka jana ikiwashirikisha washindani 614. 971912