IQNA

Kasisi Terry Jones aunga mkono kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani

16:44 - March 17, 2012
Habari ID: 2293097
Kasisi wa Marekani aliyeivunjia heshima Qur'ani Tukufu Terry Jones amewapongeza askari wa nchi hiyo huko Aghanistan kwa kuchoma moto nakala za kitabu kitakatifu cha Qur'ani katika kituo cha anga cha Bagram.
Kasisi Terry Jones kiongozi wa Kanisa la Dove World Outreach Center lenye wafuasi 50 katika jimbo la Florida ambaye mwaka 2010 alitangaza siku ya kuchomwa Qur'ani Tukufu, ameunga mkono kitendo cha askari wa Marekani huko Afghanistan cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu na kutangaza kuwa ana nia ya kuanzisha kampeni ya kimataifa ya kuchomwa moto kitabu kitakatifu cha Waislamu.
Kasisi huyo mbaguzi amedai kuwa haki za Wakristo haziheshimiwa Mashariki ya Kati na kusisitiza kuwa ataanzisha kampeni ya kimataifa ya kuchomwa moto Qur'ani na picha zinazodaiwa kuwa ni Mtume Muhammad (saw). 972905
captcha