Gazeti la al Youm al Sabii linalochapishwa nchini Misri limeandika kuwa mashindano hayo yanafanyika kwa shabaha ya kuwahamasisha watoto na vijana wa Uholanzi na Waarabu wanaoishi nchini humo kuhifadhi Qur'ani Tukufu.
Msimamizi wa Jumuiya ya Iqra nchini Uholanzi Mustafa al Tamna amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika katika ngazi 8 kwa makundi ya watoto wenye umri tofauti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 20.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa wavulana na mabinti 170 waliohifadhi Qur'ani Tukufu wanashirika katika mashindano hayo. 972893