Hayo yamesemwa Tehran na Spika ya Majlisi wa Ushauri ya Kiislamu (Bunge) Dakta Ali Larijani alipokutana wanaharakati wa tawi la Asia la msafara wa kimataifa wa 'Hadi Baitul Muqaddas'. Naye mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa Ali Akbar Velayati amehutubia msafara huo na kusema, 'baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel alitimuliwa Iran na mahala pake kuchukuliwa na ubalozi wa Palestina ambao hadi sasa unaendeleza shughuli zake Tehran'.
Velayati amesesma Iran itaendelea kuunga mkono harakati za ukombozi Palestina. Ameongeza kuwa mwamko wa Kiislamu katika eneo la Mashariki ya Kati umeongeza matumaini ya kukombolewa Palestina na hasa Quds Tukufu kutoka kwenye makucha ya Wazayuni.
Msafara wa kimataifa wa 'Hadi Baitul Muqaddas' ulinza safari yake tarehe 9 Machi mjini New Delhi na baada ya kupita Pakistan sasa uko Iran. Wajumbe wa msafara huo wa nchi kavu wa 'Ila Baitul Muqaddas' tarehe 30 Machi watakutana nchini Lebanon baada ya kupitia Uturuki. Msafara kama huo kutoka Ulaya umewasili nchini Jordan na ule kutoka Afrika pia tayari umeshafika Misri.
Lengo la misafara hiyo ni kukutana katika maeneo yaliyo karibu zaidi na mji mtukufu wa Quds ulioko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
973298