Mkurugenzi wa Darul Qur'ani ya mji wa Nasiriyya Raad Adnan amesema kuwa kikao hicho kitafanyika katika Msikiti wa Jamia na Hussainiya ya Ahlul Bait (as) katika mji huo. Amesema kikao hicho pia kitamuenzi Qarii mashuhuri wa Iraq Ali Ismail al Bayati.
Qarii huyo alishiriki katika masomo ya Qur'ani ya Kituo cha Qur'ani cha Sayyida Ruqayya katika mji mtakatifu wa Qum na ameshiriki pia kwenye mashindano mengi ya kitaifa na kimataifa ya Qur'ani Tukufu.
Raad Adnan amesema kuwa al Bayati ambaye alishika nafasi ya kwanza katika mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ataanza kufanya kazi katika Darul Qur'ani ya mji wa Nasiriyya kama mwalimu wa kituo hicho. 973498