IQNA

Polisi ya Tunisia yaanza uchunguzi kuhusu watu waliovunjia heshima Qur'ani Tukufu

16:26 - March 18, 2012
Habari ID: 2293604
Polisi ya mji wa Ben Gardan nchini Tunisia imetangaza kuwa imeanza uchunguzi mkubwa wa kuwasaka watu waliovunjia heshima Qur'ani Tukufu katika mji huo.
Tovuti ya espacemanager imeripoti kuwa, watu waliokwenda kusali Swala ya Alfajiri katika mji wa Ben Gardan Ijumaa iliyopita waligundua kuwa nakala za Qur'ani Tukufu zimevunjiwa heshima na nara zinazokejeli Uislamu zimeandikwa katika kuta na milango ya eneo hilo la ibada.
Katibu Mkuu wa chama cha an Nahdha katika eneo hilo amelaani kitendo hicho kiovu na kutangaza kuwa polisi imeanzisha uchunguzi wa kuwasaka watu waliohusina na uhalifu huo.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Ben Gardan pia jana walifanya maandamno wakilaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na maeneo ya ibada ya Waislamu.
Maandamano hayo yamevishirikisha vyama vya kisiasa, wanachama wa jumuiya za kiserikali na zisizo za serikali na taasisi mbalimbali za Kiislamu na wamewataka Waislamu kuwa watulivu na kulipa jeshi la polisi fursa ya kuwasaka watu waliohusika na uhalifu huo. 973754
captcha