Rais Ahmadinejad pia ametoa salamu za kheri na fanaka kwa taifa lote la Iran na jamii nzima ya mwanaadamu kwa mnasaba wa kuwadia msimu wa machipuo na sikukuu ya Nowruz.
Rais Ahmadinejad amesema, mwaka uliopita ulijaa matukio mengi ya furaha na ushindi kwa taifa la Iran na jamii nzima ya mwanaadamu.
Amesema mwaka uliopita wa 1390 Hijria Shamsia ulishuhudia harakati ya kasi ya taifa la Iran katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kisayansi, kiviwanda, kiteknolojia na kisiasa. Amesema kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu SWT, mwaka huu, Iran itaendelea na harakati yake katika mkondo huo wa ustawi kwa kasi ya juu zaidi.
974394