IQNA

Redio Qur'ani ya Cairo yatimiza miaka 48

12:12 - March 25, 2012
Habari ID: 2294533
Redio Qur'ani ya Cairo Misri leo imetimiza umri wa miaka 48 tangu iasisiwe.
Gazeti la al Youm al Sabi limeandika kuwa, Redio Qur'ani ya Cairo saa mbili na dakika 26 asubuhi ya leo imetimiza umri wa miaka 48 na sherehe za kuadhimisha tukio hilo zimehutubiwa na karii mashuhuri wa Misri Sheikh Mahmoud Khalil al Hisari akieleza jinsi kanda ya kiraa ya kwanza kabisa ya tartili ya Qur'ani Tukufu ilivyorushwa hewani kupitia redio hiyo.
Baadaye Redio Qur'ani ya Cairo imerusha hewani hotuba ya Sheikh Mustafa Ismail akieleza jinsi alivyopata umashuhuri na uanachama katika redio hiyo.
Redio Qur'ani ya Cairo nchini Misri ilianza kazi zake tarehe 25 Machi mwaka 1964 ikirusha hewani matangazo kwa muda wa masaa 14 kwa siku na miezi miwili baadaye ilianza kutangaza kwa masaa 24 kwa siku. 974996
captcha