Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Teolojia, Shirikisho la Jumuiya za Qur'ani na Taasisi ya Maimamu wa Swala za Jamaa wa Tunisia imewataka raia wa nchi hiyo kufanya maandamano leo kwa ajili ya kupinga vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.
Washiriki katika maandamano hayo watatangaza upinzani wao mkubwa dhidi ya kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na kuandikwa nara zinazokebehi Uislamu katika kuta na milango ya Msikiti wa Ben Gardan.
Ijumaa iliyopita watu waliokwenda kutekeleza ibada ya Swala ya Alfajiri katika msikiti huo walikuta nakala za Qur'ani zikiwa zimevunjiwa heshina na maandishi yanayouvunjia heshima Uislamu yakiwa yameandikwa katika kuta za msikiti huo.
Jumamosi ya wiki iliyopita wakazi wa mji wa Ben Gardan walifanya maandamano makubwa wakipinga kitendo hicho kiovu na kulitaka jeshi la polisi kuwasaka watu waliotenda uhalifu huo. 974732