IQNA

Makumbusho ya Houston Yaonesha Karne za Sanaa ya Qur’ani Katika Maonyesho Mapya

17:29 - September 03, 2025
Habari ID: 3481176
IQNA – Jumba la Makumbusho ya Sanaa la Houston, jimbo la Texas nchini Marekani, linaandaa maonyesho ya nakala za Qur’ani kutoka maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.

“Bahari ya Wino, Msitu wa Kalamu: Sanaa ya Qur’ani katika Mkusanyiko wa Hossein Afshar” ni maonyesho maalum yanayoadhimisha uzuri wa nakala za Qur’ani, na yataendelea kuonyeshwa hadi tarehe 28 Juni, 2026.

Maonyesho haya yanazingatia kazi bora kumi na mbili kuanzia karne ya 7 hadi ya 19, yakifichua mbinu na uzuri wa uandishi wa nakala za kifahari za Qur’ani kutoka maeneo mbalimbali ya Kiislamu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 1,200.

Mambo ya Kuvutia Yanayojumuishwa: ni pamoja na

1. Ukurasa wa karne ya 7 kutoka nakala ya Qur’ani iliyoandikwa kwa maandishi ya Hijazi juu ya ngozi ya mnyama kutoka Saudi Arabia—moja ya nakala za awali kabisa za Qur’ani, ambapo ni kurasa na vipande tu vilivyosalia. Nakala ya Qur’ani yenye mapambo ya kuvutia kutoka Iran, iliyoandikwa mwaka AH 1260 (1844–45), ikiwa imesainiwa na kuandikwa na mwanakaligrafia Mir ʿAbd al-Karim Muhammad Sadiq al-Husayni al-Yazdi. 

2. Kazi ya kisasa ya Pouran Jinchi iitwayo Tajvid Red 2 (2009), kazi ya wino juu ya karatasi inayotafsiri kipengele muhimu cha Qur’ani—tajwid, yaani usomaji sahihi—ikisisitiza uritmia na uigizaji wa kitendo cha uandishi, na kugeuza mtazamo wa mtazamaji kutoka maana ya neno hadi sauti yake.

3. Kazi ya mwanakaligrafia mahiri Haji Noor Deen iitwayo Ayat al-Kursi Scroll (2015), inayochanganya nidhamu ya kalamu ya mianzi ya Kiislamu na mtindo wa brashi ya Kichina katika maandishi ya Kiarabu ya Sini, kuandika Ayat al-Kursi—aya maarufu ya Qur’ani inayosomwa na kuandikwa sana, ikiaminika kuleta ulinzi kwa nyumba na familia.

Makumbusho ya Sanaa ya Houston yapo katika eneo la Makumbusho la Houston, Texas. Mkusanyiko wake wa kudumu unahusisha historia ya zaidi ya miaka 5,000 na kazi takriban 80,000 kutoka mabara sita. Kwa ukubwa wa kumbi za maonyesho, ni makumbusho ya pili kwa ukubwa katika Amerika.

3494459

captcha