IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya al Aqsa kufanyika Palestina

12:19 - March 26, 2012
Habari ID: 2294802
Mashindano ya kimataifa ya hifdhi na kiraa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika mwezi wa Ramadhani wa mwaka huu chini ya usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina.
Mashindano hayo yataanza tarehe 10 Ramadhani na kuendelea hadi Ramadhani 17.
Waziri wa Wakfu wa Palestina Mahmoud al Habash amesema mashindano hayo yatawashirikisha wawakilishi wa nchi mbalimbali za Kiarabu na Kiislamu na lengo lake ni kueneza utamadunbi wa Qur'ani.
Al Habash ameongeza kuwa, mashindano hayo ni katika utekelezaji wa sera za wizara yake za kukipa umuhimu kitabu cha Mwenyezi Mungu, kuwalingania vijana suala la kuimarisha uhusiano wao na maneno ya Muumba na kulea kizazi chenye utamaduni wa Qur'ani Tukufu.
Waziri wa Wakfu wa Palestina amesisitiza kuwa mashindano hayo yamepewa jina la al Aqsa kwa shabaha ya kuimarisha uhusiano wa Waislamu na suala muhimu zaidi la ulimwengu wa Kiislamu yaani Quds Tukufu na Msikiti wa al Aqsa.
Mashindano hayo yanasimamiwa na kamati maalumu za wataalamu wa sayansi ya Qur'ani kutoka nchi mbalimbali. 975259

captcha