IQNA

Nchi 41 zaalikwa kushiriki mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Jordan

12:32 - March 26, 2012
Habari ID: 2294808
Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan imetangaza kwamba nchi 9 tayari zimetangaza kwamba zitashiriki katika mashindano ya 20 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini humo.
Waziri wa Wakfu wa Jordan Abdulsalam al Ibadi amesema kuwa wizara yake imezialika nchi 41 kushiriki katika mashindnao hayo. Ameongeza kuwa tayari nchi 9 zimetangaza kuwa wawakilishi wao watashiriki katika mashindano hayo.
Amesema kuwa mashindano hayo ya kimataifa ya hifdhi, kiraa na tafsiri ya Qur'ani ya wanaume yatafuatiwa na ya wanawake.
Al Ibadi amesema Wizara ya Wakfu ya Jordan imezitaka nchi za Saudi Arabia, Sudan na Algeria kutuma majaji wa mashindano ya wanaume na kwamba majaji wa mashindano ya wanawake watatoka nchi za Saudi Arabia na Imarati.
Waziri wa Wakfu wa Jordan amesema washindi wa kiume wa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani wataenziwa katika siku za Lailatul Qadr kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhani na washindi wa kike wataenziwa hapo baadaye. 974976


captcha