Mtandao wa felesteen.ps umeripoti kuwa, Mufti Mkuu wa Quds na Palestina Sheikh Muhammad Hussein ametoa taarifa akitaka kusitishwa uuzwaji wa nakana hizo za Qur'ani Tukufu kutokana na makosa yake ya kichapa.
Taarifa hiyo imesema kuwa ukurasa wa 303 wa nakala hiyo ya Qur'ani una makosa ya kichapa na neno «سببا» limekosewa na kuandikwa «سيبا».
Sheikh Muhammad Hussein amesema katika taarifa hiyo kwamba, nakala hiyo ya Qur'ani ilichapishwa na kiwanda cha uchapishaji cha al Iman katika eneo la Mansura nchini Misri na iliidhinishwa na Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiislamu ya al Azhar tarehe 01/08/2006.
Mufti wa Palestina amezitaka maktaba na watu wote wanaomiliki nakala hizo za Qur'ani kuzikabidhi kwa Darul Iftaa ya Palestina ili hatua za dharura zichukuliwe.
Amesisitiza pia juu ya udharura wa kuwa makini sana katika kazi ya uchapishaji wa nakala za Qur'ani tukufu na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu ameilinda Qur'ani na uposhaji kwa msingi huo sisi pia tunapaswa kumridhisha Allah kwa kufanya bidii katika kulinda kitabu chake. 976949