Kwa mujibu wa tovuti ya mauritanie-web, kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Ustawi wa Sekta Binafsi Mauritania na Baraza Kuu la Mfumo wa Banki za Kiislamu. Wasomi wanaotazamiwa kuhudhuria kongamano hilo ni kutoka Mauritania, Morocco, Libya, Algeria na Tunisia.
Masuala yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na uwezo wa nchi za Kiarabu za eneo la Maghreb katika kustawisha uchumi wa Kiislamu na stratejia za kuwavutia wawekezaji wa kigeni. Washiriki pia watajadili nafasi ya uchumi wa Kiislamu katika maendeleo ya mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
Kikao hicho kimetajwa kuwa fursa kwa wataalamu wa uchumi wa Kiislamu kwani wataweza kubadilishana mawazo na uzoefu. Awamu ya kwanza ya kikao hicho ilifanyika Julai 15-16 2011 nchini Tunisia.
976858