Maonyesho hayo yanalenga kuangazia umaridadi wa lugha katika Qur'ani Tukufu kupitia upambaji wa aya za Qur'ani Tukufu.
Maonyesho hayo yanaonyesha kazi za mwana kaligrafia wa Syria Obeida al Banki ambaye alianda 'Mushafu wa Qatar. Wengine wanaoonyesha kazi zao hapo ni Mqatari Wadha al-Suleiti, Hala Saleh al-Sayyid kutoka Syria, Mona Khalifa al-Kubaisi, Mohamed Salem al-Mahmoud, Fatima Ali, Laila al-Fuhaid, Maryam al-Fuhaid, Rawdha Bujsoum and Sheikha al-Kuwari wote kutokaQatar, pamoja na kazi za Mary Catherine kutoka Ufaransa and Harumi Horekoumi kutoka Japan.
Wizara ya WQakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imesema maonyesho kama hayo ni ishara kuwa wizara hiyo ina lengo kueneza utamaduni wa Qur'ani na Lugha ya Kiarabu.
977002