IQNA

Tunisia haitaanzisha uhusiano na Israel

14:22 - April 03, 2012
Habari ID: 2296622
Kiongozi wa chama cha Kiislamu cha An Nahdha cha Tunisia amesema hakuna uwezekano hata kidogo wa nchi yake kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Akizungumza Aprili Mosi katika eneo la Bajah kaskazini magharibi mwa Tunisia, Rashid al Ghanushi amesema: 'kuanzishwa uhusiano kati ya Tunisia na utawala haramu wa Israel ni jambo lisilowezekana.'
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwa ajili ya kutangaza mfungamano na Wapalestina kwa mnasaba wa 'Siku ya Ardhi', Ghanushi amesema, 'Watunisia wana matatizo na Wazayuni na si Mayahudi'.
Ameongeza kuwa rais aliyetimuliwa madarakani nchini Tunisia Zain al Abidin ben Ali aliwasaliti Wapalestina kwani alikuwa ni kibaraka na mamluki wa Wazayuni.
Machi 30 huadhimishwa huko Palestina kama Siku ya Ardhi. Siku hii ni kumbukumbu ya hujuma ya kinyama ya jeshi la utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakilalamikia sera za ardhi za Tel Aviv mwaka 1967.
Mwaka huu katika siku hii maandamano ya kuunga mkono Palestina yalifanyika katika maeneo ya mipakani ya nchi zinazopakana na Palestina inayokaliwa kwa mabavu kama vile Lebanon, Misri, Jordan na Syria. Maandamano hayo yaliwakutanisha pamoja wanaharakati wa kimataifa walio katika msafara wa 'Hadi Beitul Muqaddas.'
977042
captcha