IQNA

Awamu ya mwisho ya mashindano ya Qur'ani barani Ulaya kufanyika Ujerumani

21:11 - April 04, 2012
Habari ID: 2298139
Awamu ya mwisho ya mashindano ya 24 ya Qur'ani Tukufu barani Ulaya itafanyika tarehe 8 Aprili katika mji wa Wuppertal nchini Ujerumani.
Tovuti ya 'igmg' imeripoti kuwa, awamu ya mwisho ya mashindano ya 24 ya Qur'ani Tukufu yameliyopewa jina la «فَأَیْنَ تَذْهَبُونَ» (Mnakwenda Wapi?) itasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Millî Görüş na kuwashirikisha wasomaji bora kutoka nchi mbalimbali za Ulaya.
Mashindano hayo yanawashirikisha washindani wenye umri wa kati ya miaka 10 na 18.
Washiriki katika mashindano hayo walishinda mashindano ya awali katika miji, nchi na kanda zao na wakachaguliwa kushiriki katika awamu ya mwisho ya mashindano hayo.
Ratiba nyingine za mashindano hayo ni pamoja na maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu, maonyesho ya vitabu vya kidini kwa lugha mbalimbali za Ulaya, maonyesho ya shughuli za Jumuiya ya Millî Görüş katika nchi mbalimbali duniani na uzinduzi wa tovuti ya mashindano ya Qur'ani Tukufu barani Ulaya kwa lugha mbili za Kituruki na Kijerumani. 978320
captcha