IQNA

Wanawake milioni moja wasio Waislamu wavaa ushungi katika Facebook

12:43 - April 05, 2012
Habari ID: 2298298
Wanawake milioni moja wasio Waislamu wameamua kuvaa ushungi na kujitokeza katika ukurasa wa Facebook kama hatua ya kupinga mauaji ya Shaima Alawadi, mwanamke Muislamu wa Iraq aliyeuawa na watu wasiojulikana katika jimbo la Florida nchini Marekani kwa sababu ya kutumia vazi la staha la hijabu.
Gazeti la Huffington Post limeripoti kuwa wanawake wengi wasio Waislamu nchini Marekani wameweka picha zao wenyewe wakiwa wamevaa ushungi katika ukurasa wa Facebook wa "Hijabu Milioni moja kwa ajili ya Shaima".
Maiti ya Shaima aliyekuwa na umri wa miaka 32 na mama wa watoto watano ilikutwa nyumbani kwake katika mji wa El Cajon katika jimbo la California tarehe 21 Machi. Mwanamke huyo Muislamu alifariki dunia kutokana na majeraha makali huku akiwa amelala kwenye zinga la damu. Kandokando ya maiti yake kulikuwa na ujumbe unaosema: "Gaidi, rudi nchini kwako."
Baada ya tukio hilo kumefanyika maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani ambayo yamepewa jina la "Hijabu na Jaketi yenye Kofia".
Neno jaketi yenye kofia linaashiria mauaji ya kijana mwenye asilia ya Afrika raia wa Marekani Trayvon Martin ambaye tarehe 26 Februari aliuawa kwa kupigwa risasi na askari mlinzi huko Florida. Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasisitiza kuwa mauaji hayo yamefanyika kwa sababu za kibaguzi. 978592

captcha