Akizungumza kabla ya kuanza hotuba za Sala ya Ijumaa mjini Tehran wiki hii, Hujjatul Islam Sayyid Yadullah Shirmardi ameashiria umuhimu wa Sala ya Ijumaa na kuongeza kuwa kamati yake inapanga kuchapisha kitabu kuhusu umuhimu na sheria za Sala ya Ijumaa. Hujjatul Islam Sayyid Shirmardi ameongeza kuwa Kamati ya Sala ya Ijumaa Tehran itabuni Idara ya Kimataifa ambayo itakuwa na jukumu la kusambaza hotuba za Sala ya Ijumaa ya Tehran kote duniani.
Ametoa wito kwa wananchi na taasisi zote nchini Iran kufanya juhudi kufanikisha kaulimbiu ya mwaka huu wa 1391Hijria Shamsia ambayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliitaja kuwa ni 'Uzalishaji wa Kitaifa, Kuunga Mkono Kazi wa Rasilimali ya Kiirani'.
979332