IQNA

Iran kuanzisha tovuti ya Qur'ani na Tiba

16:48 - April 07, 2012
Habari ID: 2299265
Kituo cha Qur'ani cha Wizara ya Elimu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kimetangaza kuwa kitaanzisha tovuti kamili ya Qur'ani na Tiba katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.
Akizungumza na IQNA, mkuu wa kituo hicho Mahdi Salehi amesema: "Duru ya 17 ya Tamasha ya Qur'ani ya wanachuo wa vyuo vikuu vya kitiba nchini Iran pia inatazamiwa kufanyika baadaye mwezi Mei.'
'Kuandaa awamu ya pili ya Kongamano la Utafiti wa Qur'ani na Tiba pamoja na kuanzisha kitengo cha kimataifa cha tamasha hiyo ni kati ya program tulizoandaa mwaka huu,' ameongeza.
Kuhusu tovuti ya Qur'ani na Tiba, Salehi amesema itakuwa na nafasi kubwa katika kuwasaidia watafiti wa taaluma hii. Ameongeza kuwa vyuo vikuu vyote vya kitiba nchini Iran vinapaswa kuandaa vikao na makongamano kuhusu 'utafiti wa Qur'ani na tiba'.
977156
captcha