Naibu Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait amesema kuwa nchi 50 duniani zitashiriki katika mashindano ya kimataifa ya hifdhi, kiraa na tajwidi ya Qur'ani Tukufu, Tuzo ya Kuwait.
Adil al Falah ameviambia vyombo vya habari kwamba nchi 56 zilialikwa katika mashindano hayo na kwamba nchi 50 zimetangaza kwamba ziko tayari kushiriki.
Adil al Falah ameongeza kuwa wasomaji 90 watachuana katika mashindano hayo na kwamba nchi 46 zinazoshiriki ni za Kiislamu na nne zilizosalia ni Russia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bosnia na Serbia.
Naibu Waziri wa Wakfu wa Kuwait amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika katika sehemu nne za kuhifadhi Qur'ani nazima pamoja na tajwidi, kitengo cha visomo saba, kiraa na tajwidi na kitengo cha teknolojia bora zaidi ya kuhudumia Qur'ani. Zawadi ya mshindi wa mashindano hayo ni dinari laki moja na elfu 14 za Kuwait. 980594