IQNA

Mashindano ya 7 ya kimataifa ya Qur'ani yamalizika India

15:54 - April 08, 2012
Habari ID: 2300293
Mashindano ya saba ya kimataifa ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yamemaliza shughuli zake katika mji wa Bhopal nchini India.
Tovuti ya ibnlive imeripoti kuwa mashindano hayo yaliyosimamiwa na jumuiya ya Zinatul Qur'ani yamewashirikisha makarii 14 kutoka nchi 12.
Washiriki katika mashindano hayo walitoka nchi kama Misri, Algeria, Syria, Malaysia, Indonesia, Morocco, Uturuki, Iraq na Bangladesh.
Washriki kutoka nchi za Algeria, Misri na Iraq wametambuliwa kuwa wasomaji bora zaidi wa mashindano hayo.
Hatibu wa Msikiti wa al Aqsa Ikrima Sabri alikuwa mgeni wa fahari wa mashindano hayo na aliongoza Sala ya Ijumaa ya Msikiti wa Bhopal. 980229


captcha