IQNA

Kasisi wa Marekani aivunjia heshima tena Qur'ani Tukufu

16:06 - April 08, 2012
Habari ID: 2300304
Kasisi Terry Jones wa Marekani aliyewahi kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu Jumamosi ya jana alikusanyika na wafuasi wake kadhaa mbele ya Kituo cha Kiislamu cha mji wa Dearborn katika jimbo la Michigan huko Marekani.
Kasisi huyo muovu aliwahutubia watu kadhaa kwa karibu saa moja mbele ya msikiti huo mkubwa zaidi katika eneo la kaskazini mwa Marekani.
Akitumia kipaza sauti, Kasisi Jones ameshambulia taasisi za dini ya Kiislamu na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) na kitabu cha Qur'ani Tukufu.
Mkusanyiko huo umefanyika chini ya usimamizi wa polisi na bila ya mapigano. 980838




captcha