IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran kuanza 26 Rajab (17 Juni)

14:53 - April 09, 2012
Habari ID: 2300843
Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ambayo hufanyika Iran kila mwaka yanatazamiwa kuanza tarehe 26 Rajab sawiya na 17 Juni mwaka huu ambapo nchi 95 zimealikwa kushiriki.
Kwa mujibu wa Shirika la Wakfu la Iran Mashindano ya 29 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika sambamba na maadhimisho ya Kubaathiwa Mtume Mtukufu Muhammad Al Moustafa SAW.
Akizungumza na IQNA, mkuu wa masuala ya mashindano katika Shirika la Wakfu la Iran Bw. Wali Yar-Ahmadi amesema maqarii na mahufadhi kutoka baadhi ya nchi hizo 95 tayari wameshaarifisha washiriki. Amesema washiriki si kutoka nchi za Kiislamu tu bali ni kutoka maeneo yote duniani zikiwemo zile zenye Waislamu wachache. Ameongeza kuwa kila nchi inaweza kuarifisha qarii na hafidhi mmoja tu.
Mwaka jana wawakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika vitengo vya hifdhi na qiraa walishika nafasi za kwanza katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yaliyowashirikisha watu 96 kutoka nchi 61 duniani.
Mshiriki kutoka nchini Tanzania Ibrahim Ramadhan Shaaban aliibuka wa tano katika hifdhi.
981351

captcha