IQNA

Mashidano ya Kitaifa ya Qur'ani kufanyika Misri

14:53 - April 09, 2012
Habari ID: 2300861
Wizara ya Wakfu ya Misri imesema inapanga kuandaa mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Qur'ani katika mustakabali usio mbali nchini humo.
Kwa mujibu wa tovuti ya al Ahram, mashindano hayo yatafanyika chini ya kaulimbiu ya 'Kuhimiza Mashidano ya Qur'ani'.
Naibu Waziri katika Wizara ya Wakfu anayeshughulikia masuala ya Qur'ani Sheikh Foa'aad Abdu-Azim amesema usajili wa washiriki unaendelea katika vituo vyote vya wakfu nchini humo.
'Kamati maalumu za Qur'ani zinazojumuisha wataalamu na maafisa wa Awqaf zitawateua washiriki,' amesema.
Ameongeza kuwa wale wanaopata wanaopata pointi 90 kati ya 100 katika awamu ya kwanza wataingia awamu ya pili na washindi hapo watashiriki katika mashindano ya kitaifa na hatimaye ya kimataifa.
Mashindano mengine ya Qur'ani maalumu kwa Maimamu misikitini pia yatafanyika hivi karibuni nchini Misri.
980846
captcha