Tovuti ya Aman Trust imeripoti kuwa, mashindano hayo yatasimamiwa na taasisi ya elimu ya The Amal Trust ya Uingereza kwa kushirikiana na Wizara ya Wakfu ya Qatar.
Mashindano hayo yatafanyika katika sehemu tano za kuhifadhi Qur'ani nzima, juzuu 20, juzuu 15, juzuu 10 na juzuu 5.
Wavulana na wasichana wenye chini ya umri wa miaka 25 wa Uingereza watashiriki katika mashindano hayo yatakayoendelea kwa kipindi cha siku mbili.
Washindi wa kila kundi watatunukiwa zawadi za fedha taslimu. 981948