Mwalimu wa lugha ya Kiarabu wa chuo hicho Ramadhan Mustafaov amesema kuwa mafunzo hayo ya Qur'ani na lugha ya Kiarabu yanahudhuriwa na walemavu wa macho kutoka jamhuri za Ingushetia, Dagestan, Chechnia na Russia.
Ameongeza kuwa Chuo cha Arsanov ndicho kilichobunu fikra ya kuanzisha mafunzo hayo na ndicho kinachoyagharimia.
Ramadhan Mustafanov amesema kuwa kwa kutilia maanani kwamba mafunzo hayo yamewavutia watu wengi wenye ulemavu wa macho, chuo cha Kiislamu cha Arsanov kimeamua kutoa masomo hayo muda wote wa mwaka mzima. 981870