IQNA

Israel yawazuia Waislamu kuingia Haram ya Nabii Ibrahim

19:01 - April 09, 2012
Habari ID: 2301236
Askari wa utawala haramu wa Israel jana Jumapili waliwazuia Waislamu kuingia katika Haram ya Nabii Ibrahim katika mji wa al Khalil kwa kisingizio cha sherehe za Pasaka.
Shirika rasmi la habari la Palestina limetangaza kuwa askari wa utawala haramu wa Israel jana walifunga kikamilifu Haram ya Nabii Ibrahim na kuwazuia Waislamu kuingia humo.
Uamuzi huo wa Israel uliwazuia Waislamu kutekeleza ibada ya Swala kwenye eneo hilo takatifu na kuruhusiwa Wayahudi kuingia humo.
Mkurugenzi wa Wakfu wa Palestina Zaid Jaafar amesema kuwa Haram ya Nabii Ibrahim (as) ni mali ya Waislamu wote duniani na walowezi wa Kizayuni hawana haki ya kulidhibiti eneo hilo tukufu.
Haram ya Nabii Ibrahin ni jengo lililoko katikati mwa mji wa al Khalil umbali wa kilomita 44 kutoka Baitul Muqaddas na wafuasi wa dini zote za mbinguni wanaamini kwamba mwili wa Nabii Ibrahim (as) umezikwa mahala hapo. 981713

captcha