IQNA

Iran kuandaa tamasha kubwa zaidi duniani ya Qur'ani za Dijitali

17:28 - April 10, 2012
Habari ID: 2301591
Tamasha ya Qur'ani za Dijitali yenye anwani ya 'Tamasha ya Imani ya Kitaifa ya Qur'ani' inatazamiwa kufanyika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utamaduni ya Soroushe Mehra kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu na Shirika la Simu za Mkononi nchini Iran MCI.
Mkuu wa Shoroushe Mehr Bw. Ibrahim Bahadori amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, 'Hii inaaminika kuwa tamasha kubwa zaidi ya Qur'ani za dijitali kuwahi kufanyika katika ulimwengu wa Kiislamu ambapo wanafunzi milioni 12 wanatazamiwa kushiriki kwa kutumia kompyuta na simu za mkononi.'.
Amesema wanafunzi hao watapokea programu za kompyuta na kupata maelezo ya kuzitumia kupitia kipindi maalumu kitakachorushwa hewani katika Kanali ya Kielimu ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB).
Akisisitiza umuhimu wa kutumia teknolijia za kisasa katika uga wa elimu, Ibrahim Bahadori amesema programu hizi zitaweza kutathmini uwezo wa qiraa na hifdhi wa washiriki na kuwapa pointi.
981536
captcha