IQNA

Mashindano ya kiraa ya Qur'ani kufanyika Russia

20:25 - April 10, 2012
Habari ID: 2302113
Ofisi ya upashaji habari ya Idara ya Masuala ya Waislamu wa Russia imetangaza kuwa mashindano ya kiraa ya Qur'ani Tukufu yatafanyika katika mji wa Tolyatti katika siku chache zijazo.
Idara hiyo imesema kuwa tarehe maalumu ya kufanyika mashindano hayo inachunguzwa na kuna uwezekano yakafanyika katika msimu wa joto ujao katika vitengo vya kiraa na hifdhi ya Qur'ani pamoja na adhana.
Ofisi hiyo imetangaza kuwa watu wote wanaweza kushiriki katika mashindano hayo na kwamba washiriki wengi ni wanafunzi wa shule za kieneo.
Katika siku zijazo pia msikiti mkuu wa mji wa Tolyatti utakuwa mwenyeji wa masomo ya muda ya hifdhi ya Qur'ani Tukufu na misingi ya Uislamu. 982767

captcha