IQNA

Sira na mwenendo wa Ahlul Bait (as) kubainishwa Kenya

14:11 - April 11, 2012
Habari ID: 2302780
Sira na mwenendo wa kimaadili wa Ahlul Bait wa Mtume (saw) utabainishwa katika semina iliyopangwa kufanyika katika Msikiti wa Safa kwenye kisiwa cha Lamu nchini Kenya. Semina hiyo itafanyika Ijumaa ijayo.
Mwakilishi wa IQNA kanda ya Afrika amesema kuwa semina hiyo itafanyika tarehe 13 Aprili saa tatu asubuhi na kuendela hadi kabla ya Sala ya Ijumaa. Amesema semina hiyo itahutubiwa na maulamaa kadhaa akiwemo mwanazuoni mashuhuri Sayyid Aidarus.
Kabla ya kuanza semina hiyo Karii bora wa kisiwa cha Lamu Abdul Ghani Othman al Khatib atasoma aya za Qur’ani na baada ya hapo mahatibu na maulama wa kidini watatoa hotuba wakizungumzia sira na mwenendo wa kiakhlaki wa Ahlul Bait (as). 983410
captcha