IQNA

Mashindano ya kimataifa ya Qur’ani ya Kuwait yaanza leo

14:54 - April 11, 2012
Habari ID: 2302820
Duru ya tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Hifdhi, Kiraa na Tajwidi ya Qur’ani Tukufu Tuzo ya Kuwait yameanza leo Jumatano nchini humo.
Gazeti la al Rai linalochapishwa nchini Kuwait limeripoti kuwa, mashindano hayo yanayosimamiwa na Amir wa nchi hiyo Sheikh Sabah al Ahmad yataendelea kwa kipindi cha wiki moja.
Wasomaji Muhammad Javad Muhammadi na Redha Golshahi kutoka Iran wanashiriki katika mashindano hayo.
Nchi 46 za Kiislamu na 4 zisizo za Kiislamu ambazo ni Russia, Jamhuri ya frika ya Kati, Bosnia na Serbia pia zinashiriki katika mashindano hayo.
Washindi wa kwanza wa mashindano hayo watatunukiwa zawadi ya dinari laki moja na elfu 14 za Kuwait.
Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Qur’ani ya Kuwait Khalid Bugheit amesema kuwa mashindano hayo yanafanyika katika vitengo vinne vya hifdhi ya Qur’ani nzima pamoja na tajwidi, kiraa saba, kiraa na tajwidi ya Qur’ani na teknolojia bora zidi ya kuhudumia Qur’ani Tukufu. 982289

captcha